RC MAKONDA AONGOZA SALA MAALUM KUOMBEA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA





Na Prisca Libaga Maelezo Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa mara zote wanamuhusisha Mwenyenzi Mungu kwenye maisha yao ili awanusuru na madhila mbalimbali ikiwemo ajali, vifo vya ghafla na kudumaa katika ustawi.

Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Disemba 09, 2024 akiwa kwenye Mnara wa Saa Jijini Arusha wakati wa matembezi ya sala maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha yaliyojumuisha viongozi wa Dini zite mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara.

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa wakazi wa Arusha kuwa makini na watu wanaowapa nafasi za Uongozi, kwa kuhakikisha Viongozi wanaowachagua ama kuwateua wanatokana na madhabahu ya Mungu kwa kuzishika amri na maelekezo ya Mungu.
Previous Post Next Post