SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU NBC TANZANIA BARA






Simba SC imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Disemba 24, 2024 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, uliopo Mwenge, Dar es Salaam

JKT Tanzania walifanikiwa kuwatuliza Simba SC kwa takriban dakika zote tisini za mchezo lakini hata hivyo, kwenye zile sita za nyongeza, wakafanya madhambi na Simba wakapata mkwaju wa penalti na Jean Ahoua akaweka kambani.
Kwa ushindi huo mwembamba, Simba ameendelea kujikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na alama 37 baada ya kucheza mechi 14 huku mtani wake Yanga akiwa nafasi ya pili akiwa na alama 33 akiwa amecheza mechi 13.
Previous Post Next Post