SIMBA SC YAITULIZA SINGIDA BLACK STARS






Goli la Fabrice Ngoma dakika ya 42 limewahakikishia Simba SC waendelee kujikita kileleni baada ya kuvuna alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa leo Disemba 28, 2024.

Mechi ilikuwa tafu, Singida walijaribu kutoa ushindani mkali lakini hata hivyo, Mnyama alionesha ukubwa wake na kufanikiwa kutoka na ushindi huo.

Simba Sc wamefikisha alama 40 akiwa kileleni baada ya kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza.
Previous Post Next Post