Na Mapuli Kitina Misalaba
Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (SMAUJATA) Kanda ya Ziwa imeshiriki kikao maalum cha kujadili ulinzi wa mtoto mtandaoni (Child Protection) ambacho kimeandaliwa na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.
Kikao hicho kimefanyika jijini Mwanza chini ya kauli mbiu, “Usalama wa Mtoto Mtandaoni ni Jukumu Letu, Chukua Hatua.”
Mafunzo hayo, yaliyobeba jina Lake Zone COP 2024, yamewaleta pamoja viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka Kanda ya Ziwa.
Mafunzo hayo yameendeshwa na viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Afisa Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao.
Miongoni mwa washiriki walioshiriki ni viongozi wa maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii, Dawati la Jinsia, Afisa uchunguzi wa makosa ya kimtandao, idara ya Elimu, na wawakilishi wa SMAUJATA kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, na Kagera.
Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa, Bwana Daniel Patrick Kapaya, amesema:
"Ulinzi wa watoto mtandaoni unahitaji mshikamano wa jamii nzima. Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha watoto wanatumia teknolojia kwa usalama na manufaa."
Katika mafunzo hayo, washiriki walijifunza namna ya kuboresha malezi, kuzuia matumizi mabaya ya simu za mkononi kwa watoto, na kuwajengea watoto tabia ya uwajibikaji na usalama wa mtandaoni. Pia, viongozi walitembelea Shule ya Sekondari Pamba na kuanzisha Dawati la Wanafunzi litakalosaidia kuripoti vitendo vya ukatili shuleni.
SMAUJATA imesisitiza dhamira yake ya kushirikiana na wadau mbalimbali kuboresha mifumo ya ulinzi wa watoto katika Kanda ya Ziwa.
Bw. Kileo, Afisa Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuzuia ukatili wa watoto mtandaoni.
Penina, Afisa Ustawi wa Jamii, akisisitiza jukumu la jamii katika malezi ya watoto.
Picha ya pamoja wa kwanza aliyevaa gauni la kitenge na miwani ni mwakilishi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Jiji la Mwanza, aliyeangazia changamoto za watoto shuleni ambapo wa kwanza upande wa kulia ni katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa Bwana Daniel Patrick Kapaya.
Picha ya pamoja wa kwanza upande wa kulia ni katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa Bwana Daniel Patrick Kapaya.
Picha ya pamoja wa kwanza upande wa kulia ni katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa Bwana Daniel Patrick Kapaya.
Afisa Maendeleo kutoka wizarani, akishirikiana na wadau kuboresha mifumo ya ulinzi wa watoto katika picha ya pamoja na wanafunzi.