Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Shinyanga Josephath Mwaipaja amewataka wafanya biashara ambao ndio wanaanza kufanya biashara kufika ofisi zamamlaka hiyo ili kusajili biashara zao na kupata TIN namba na hatimaye kufanya makadilio ya kodi kwa mwaka husika.
Ameyasema hayo jana alipokua akizungunza na vyombo mbalimbali katika ofisi za mamlaka hiyo.
Mwaipaja amesema kuwa mtu yeyote anapoanza kufanya biashara yoyote anapaswa kufika katika ofisi za mamlaka hiyo ili kupatiwa TIN namba na kufanyiwa makadilio jambo litakalomuwezesha kulipa kodi ambayo italiongezea taifa mapato na kuliwezesha kutekeleza miradi mbalimbali katika jamii hivyo kusaidia kuinua ustawi wa raia wake.
Wakati huo huo amewakumbusha wale wote wenye malimbikizo ya kodi kutimiza wajibu wao kwa kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kujadiliana na kuingia makubaliano ya ulipaji wa kodi bila kuathiri shughuli zao za kiuchumi, huku akuwakumbusha wa wafanyabiashara wote kulipa kodi ya awamu kwa wakati kwa mwezi huu wa disemba ifikapo disemba 31, 2024.