Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Mizengo Pinda amewataka watanzania kote nchini kuunga jitihada za maendeleo za Serikali ya awamu ya sita iliyoko chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 21 Desemba 2024 katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mwandishi Godian Dyanka cha NGUVU YA MALENGO iliyofanyika katika ukumbi wa Cavillan Social Hall Jijini Dodoma.
Mhe Pinda amesema kuwa dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuwaletea wananchi Maendeleo imeleta mabadiliko makubwa ndani na nje ya nchi kwa kuendeleza miradi ya kimkakati ya watangulizi wake katika awamu zilizopita.
"Mama Samia ni nguvu ya malengo ya nchi yetu kwa sababu alichokilenga anataka kifike na aone matokea yake" amesema Naibu Waziri mhe. Pinda
Aidha mhe Pinda amewaomba wanawake kuisadia jamii katika malezi ya watoto ili kujenga jamii iliyo staarabika kwa maendeleo endelevu ya Taifa Kiuchumi.
Kadhalika Naibu Waziri Pinda ameitaka jamii kujenga tabia ya kupenda kusoma vitabu ili kuongeza maarifa yenye mtizamo chanya wa Maendeleo ya kimaisha.