Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika kipindi cha miaka minne (2020-2024) chini ya uongozi wa Mbunge Mheshimiwa Patrobas Katambi, Jimbo la Shinyanga Mjini limepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa.
SHULE MPYA
Kabala ya mwaka 2020, kulikuwa na jumla ya shule 65 za msingi na sekondari. Hata hivyo, kwa kipindi cha miaka minne, shule mpya tisa zimejengwa, na kufikisha idadi ya shule 74. Shule hizo ni:
1. Shule ya Sekondari Mwangulumbi
2. Shule ya Sekondari Butengwa
3. Shule ya Sekondari Lubaga
4. Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga
5. Shule ya Msingi Mwamashele
6. Shule ya Msingi Mwamagulya
7. Shule ya Msingi Itongwang'olo
8. Shule ya Msingi Ibadakuli
9. Shule ya Msingi Mwasane
UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU
Katika jitihada za kuboresha na kuimarisha miundombinu ya shule, hatua zifuatazo zimechukuliwa:
Ujenzi wa vyumba vya madarasa 176 vyenye thamani ya TZS 3,520,000,000, ambapo vyote vimekamilika.
Ujenzi wa bweni katika Shule ya Msingi Buhangija, wenye thamani ya TZS 190,000,000.
Ujenzi wa mabweni manne katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga, wenye thamani ya TZS 544,000,000.
Ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Buhangija, uliogharimu TZS 650,000,000.
Hatua hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, hivyo kuinua viwango vya elimu katika jimbo hili.