WANANCHI MHONGOLO WILAYA YA KAHAMA WATOA NYUMBA KUWA KITUO KIDOGO CHA POLISI

Katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu wananchi wa Kata ya Mhongolo  Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wameamua kutoa nyumba  ili itumike kwa matumizi ya awali kama Kituo  kidogo cha Polisi wakati wakiendelea na jitihada za kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi jambo litakalo saidia kupunguza adha ya kutafuta huduma hiyo umbali mrefu.

Wananchi hao wamesema hayo Disemba 18, 2024 wakati wa uzinduzi wa kituo hicho na kusema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na Kata hiyo kutokuwa na kituo cha Polisi sambamba na kutokuwa na usalama katika maeneo yao kutokana na mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali  waliofika kwa  ajili ya shughuli za kiuchumi.

Akizungumza wakati akizindua kituo hicho Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janaeth Mgomi amewashukuru wananchi hao wakiongozwa na wafanyabiashara, wadau na vikundi vya Ulinzi shirikishi kuwezesha kupatikana kwa kituo hicho ambacho kitaongeza ufanisi  wa kazi wa Jeshi la Polisi  katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mhongolo Rita Modest amewataka wananchi wa Kata hiyo kutumia kituo hicho  kuripoti matukio ya kihalifu ili Mkoa huo  uendele kubaki salama.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mhongolo Rita Modest.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janaeth Mgomi, upande wa kushoto












Previous Post Next Post