WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZIKO YA DKT. NDUGULILE.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 03, 2024 ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile yaliyofanyika eneo la Mwongozo, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.


Viongozi wengine walioshiriki Mazishi hayo ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na viongozi wa Chama na Serikali.

Dkt. Ndugulile alifariki usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

Previous Post Next Post