Mabigwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara wameendeleza wimbi wa ushindi katika michezo ya ligi kuu baada ya kuwachapa wenyeji Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa leo Disemba 25, 2024 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji mzawa Clement Francis Mzize dakika ya 19 na 38, kiungo Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 29 na mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 63.
Kwa ushindi huo Yanga SC imefikisha pointi 36 ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mtani wa jadi Simba SC baada ya wote kucheza michi 14.
Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 16 za mechi 15 huku wakiwa nafasi ya 11.