YANGA SC YAICHAPA FOUNTAIN GATE 5 -0

Mabingwa Watetezi Yanga SC wamefanikia kuibuka na ushindi wa mabao 5 –o dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Disemba 29, 2024 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na viungo Muivory Coast , Pacome Zouzoua Peodoh mawili dakika ya 16 na 45 + 1, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 41, beki Jackson Katanga Shiga aliyejifunga dakika ya 52 pamoja na mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 88.

Kwa ushindi huo Yanga SC imefikisha pointi 39 ikimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu, ingawa imebaki nafasi ya pili nyuma ya Simba SC yenye poini 40 baada ya wote kucheza mechi 15.

Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi 20 za mechi 16 na kubaki nafasi ya 16 katika msimamo mwa ligi kuu NBC.

Previous Post Next Post