ALIYEKUWA AFISA MTENDAJI WA MTAA WA TUPENDANE KATA YA MANZESE BW. BERNARD YOHANES MHILIWA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Na Mwandishi wetu-Ubungo 

Desemba 30, 2024 Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Tupendane Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo Bw. Bernard Yohanes  Mhiliwa, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na kufunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 36014/2024.

Katika shauri hili Bw. Bernard Yohanes anashtakiwa kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tsh.124,557,900/= ikiwa ni fedha ya mapato ya ada ya taka na ulinzi shirikishi kupitia mfumo wa POS kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022

Pia ameshtakiwa kwa kosa la kuisababishia mamlaka hasara kinyume na kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza kikisomwa pamoja na kifungu cha 57(1) na 60(2) vyote vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022  

Mashtaka haya  yalisomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wakili  Sophia Nyanda mbele ya Mhe Tumsifu Gideon Barnabas, Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Ubungo.

Shauri limepangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali (PH) mahakamani tarehe 13/1/2025.

Previous Post Next Post