ALIYEKUWA MHASIBU WA KLABU YA MPIRA YA MANISPAA YA KINONDONI - KMC FC, BW. ATULINDA BARONGO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA.


Na Mwandishi Wetu -Kinondoni.

Januari 13, 2025 aliyekuwa Mhasibu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) Bw. Atulinda Barongo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni - Kinondoni Dar es Salaam na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi Namba 1099/2025.

Katika shauri hili Bw. Barongo anashtakiwa kwa kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tshs. 12,000,000/= kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyorejewa mwaka 2022

Pia ameshtakiwa kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Sura ya 329 Rejeo la 2022

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Wakili Janeth Kafuko na shauri hili linasikilizwa na Mh. Hakimu Nabwike Mbaba

Shauri limepangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali (PH) tarehe 3/2/2025.

Previous Post Next Post