𝗠𝗞𝗔𝗡𝗗𝗔𝗥𝗔𝗦𝗜 𝗖𝗝𝗥𝗘 𝗔𝗧𝗔𝗞𝗜𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗞𝗔𝗕𝗜𝗗𝗛𝗜 𝗝𝗘𝗡𝗚𝗢 𝗟𝗔 𝗪𝗜𝗭𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨









Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya China ya CRJE inayotekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kukamilisha miundombinu yote ikiwemo ya TEHAMA kuhakikisha inawezesha utoaji wa huduma kikamilifu.

Prof. Nombo ametoa agizo hilo Januari 08, 2025 wakati akikagua jengo hilo ambapo amesisitiza kuwa
makabidhiano ya jengo hilo yatafanyika Januari 19, 2025, na kwamba ni muhimu kuzingatia maelekezo yote.

Prof. Nombo pia amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu Ufundi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Fredrick Salukele kutumia timu yake ya wahandisi kufanya ukaguzi 𝘱𝘳𝘦-𝘪𝘯𝘴𝘱𝘦𝘤𝘵𝘪𝘰𝘯 kwa niaba ya watumiaji wa jengo hilo kabla ya kukabidhiwa jengo.

Katibu Mkuu huyo amemsisitiza Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanakagua kikamilifu vifaa vyote.

Previous Post Next Post