DKT. BITEKO ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA MAPINDUZI ZANZIBAR



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapimduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba, Zanzibar.

Mgeni wa Heshima katika Sherehe hizo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Viongozi wengine wa Kitaifa waliohudhuria Sherehe hizo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi wengine Wastaafu wa Serikali zote mbili.
Previous Post Next Post