HOSPTALI YA MANISPAA YA SHINYANGA YAAMZA UTOAJI WA HUDUMA YA MAZOEZI TIBA NA VIUNGO.

Na: Shinyanga MC


Hospital ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeanza utoaji huduma ya mazoezi tiba na viungo ili kuzuiwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumza leo Januari 23, 2025 Kaimu Mganga mfawidhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Moshi Lyoba amesema serikali ilitenga fedha zaidi ya Tshs milion 16 kwa ajili ya kununua vifaa tiba hiyo pamoja nakuajiri  wataalamu watatu wa Fiziotherapi kwa lengo la kuzuiwa magonjwa yasiyo ambukizwa pamoja na kuzuiwa ulemavu.

Elirumba Michaeli ni miongoni mwa wananchi walifika Katika hospitali hii kupata huduma ya viungo, ambaye ameishukuru serikali ikiongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kuleta huduma hiyo Katika Manispaa ya Shinyanga ikilenga kuondoa vifo vilvyokuwa vikisababishwa na ukosefu wa HUDUMA hiyo pamoja na ulemavu wa kudumu.

Previous Post Next Post