JAFO AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI WA KISARAWE

Mbunge wa Kisarawe ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kata za Msanga na Boga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne.

Na.Alex Sonna-KISARAWE

Mbunge wa Kisarawe ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameelezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika jimbo hilo kwenye sekta ya elimu, afya, umeme, miundombinu, na maji.

Akizungumza kwenye mikutano ya Kata za Msanga na Boga ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne, Dkt. Jafo amesema mafanikio hayo ni pamoja na vijiji vyote 83 vimefikiwa na huduma ya umeme.

Pia, amesema mafanikio mengine ni ujenzi wa shule nane za sekondari mpya na kuweka miundombinu mipya katika sekondari zote za zamani, kujengwa vituo vipya vya afya saba, maboresho makubwa ya Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na ujenzi wa zahanati kwenye vijiji mbalimbali.

"Namshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mzuri na mahiri ambao umetuletea maendeleo haya wana Kisarawe, tunayashuhudi ni mambo makubwa yamefanyika kwenye jimbo hili na yanawagusa wananchi na kuwaondolea kero walizokuwa nazo za kukosa miundombinu hii muhimu ya huduma za kijamii,"amesema.

Mbunge wa Kisarawe ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kata za Msanga na Boga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne.

Mbunge wa Kisarawe ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kata za Msanga na Boga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa miaka minne.
Previous Post Next Post