JUMUIYA YA WAZAZI CCM KATA YA NDEMBEZI YATEMBELEA KITUO CHA AFYA NGOKOLO NA KUTOA MSAADA KWA WAGONJWA

Na Elisha Petro, Misalaba Media
Viongozi na Wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha Afya Ngokolo kwa lengo la kusalimia wagonjwa na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya miaka 48 toka kuanzishwa kwa Chama hicho mwaka 1977.

Akisoma ripoti ya vitu vilivyokabidhiwa Mjumbe wa Halimashauri Kuu Kata ya Ndembezi Bwana Hashimu Issa Hashimu ametaja baadhi ya vitu vilivyokabidhiwa ambavyo ni Vinywaji,Biskuti na  Sabuni za Miche na kuiomba jamii kuguswa kusaidia watu wenye uhitaji ikiwemo wagonjwa bila ubaguzi wa chama,Kabila wala Dini.

"Sisi jumuiya ya wazazi Kata ya Ndembezi tumekuja hapa kituo cha Afya Ngokolo tumekuja hapa kwa kuambatana na viongozi wetu kuja kuwaona ndugu zetu waliowagonjwa na kuwapa pole na kukabidhi baadhi ya vitu tulivyojaaliwa kuvipata ikiwemo vinywaji (juice), Biskuti, sabuni za kufulalia na hii sio mara yetu ya kwanza bali ni desturi yetu ambayo huwa tunafanya mara kwa mara hata nje ya Ndembezi pia kwa hiyo ni waombe wanajamii wanachama wa CCM na wale wenzetu wa vyama vya upinzani waguswe kuwasaidia ndugu zetu kwani hili jambo halibagui Chama,Kabila wala Dini  bali ni la kwetu sote"

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya kituo cha Afya Ngokolo Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ngokolo Dokta Patrobas Katambi amewashukuru viongozi na wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Kata ya Ndembezi kwa moyo wa majitoleo na kutenga muda wao kufika katika kituo hicho ili kuwatia moyo wagonjwa na kuwaomba waendelea kuguswa kufika katika kituo hicho bila kuchoka.

"Nashukuru sana kwa ujio huu ambao sisi tunaona ni Baraka kwetu lakini zaidi kwa wagonjwa wetu waliopokea kile mlichokileta kwa sababu hili ni jambo jema linalompendeza Mungu na zaidi Mungu aendelee kuwaongezea nguvu na fadhira kwa sababu hiki mlichokifanya ni ukarimi mkubwa sana niwakaribishe tena kwa awamu nyingine sisi tutawapokea na tutashirikiana kwa pamoja hii ni taasisi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki lakini ni ya kwetu sote Karibuni sana hata kwa wengine watakaoguswa nao tunawakaribisha sana"

Wakizungumza na Misalaba Media baadhi ya wagonjwa wameishukuru Jumuiya ya wazazi Kata ya Ndembezi kwa vitu walivyopokea  na  kuwaomba waendelee kutenga muda wa kuendelea kuwatembelea na kuwasalimia.

"Sisi tunashukuri kwa hiki tulichokipokea ambacho ni msaada kwetu kitatusaidia katika mahitaji yetu Mungu azidi kuwabariki na tunamshukuru Rais Samia na Serikali yote kwa kuanzisha Jumuiya hizi zinatusaidia sana"

Kwa upande wake katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Ndembezi   Bi. Christiana Stanislaus Milenge ameiomba jamii kushirikiana nao katika safari ya watatembelea kituo cha watoto yatima Bushushu ifikapo siku ya jumamosi  tarehe 01.2.2025 

" Hili ni jambo letu sote niwaombe wanajamii waungane na sisi katika safari ya kwenda kituo cha watoto yatima Bushushu ambayo itakuwa siku ya jumamosi  tarehe 01.2.2025 twendeni tukawafariji watoto wetu tukawape chochote kitu tutakachokuwa nacho tuguswe kwa lengo la kuwasaidia watoto wetu 
"
Ziara hiyo ya kutembelea wagonjwa  imeongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Kata ya Ndembezi Bwana Hamis kayungila ambaye amesiaitiza Umoja, Upendo na Mshikamano wa kusaidia mkundi yenye uhitaji katika jamii na kumpongeza uongozi wa Kituo cha Afya Ngokolo kwa kupokea wito wa kufika hapo huku Katibu wa malezi Kata ya Ndembezi Bwana Peter Simon Pogoya akiwasiaitiza wazazi na waleI kuwajinikia vyema jukumu la makuzi na malezi ya watoto ili kujenga taifa bora lenye vijana wenye nguvu.

Kila ifikapo tarehe tano mwezi wa pili ya kila mwaka Chama cha Mapinduzi CCM huadhimisha sherehe za kuongeza mwaka mwingine toka kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1977  ambapo tarehe 05.2.2025 ni maadhimisho ya 48 ya kuanzishwa kwa Chama hicho.

Previous Post Next Post