Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Jumuiya ya Wazazi kata ya Ndala imeadhimisha
Wiki ya Wazazi kwa kufanya shughuli mbalimbali katika Shule ya Msingi Msufini,
ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya wazazi, shule, na jamii.
Shughuli zilizofanyika katika
maadhimisho hayo ni pamoja na:
1.
Kufanya usafi wa mazingira ndani na
nje ya shule.
2.
Kupanda miti ili kuhifadhi
mazingira.
3.
Kuchangia viroba vitatu vya unga kwa
ajili ya matumizi ya shule.
4.
Kutoa elimu ya malezi bora kwa
wazazi na wanafunzi.
5.
Kuendesha kampeni ya kupinga ukatili
wa kijinsia, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha haki za watoto na usawa wa
kijinsia.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
alikuwa Ndugu Daniel Kapaya, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi Wilaya
ya Shinyanga Mjini. Akizungumza na washiriki, Kapaya amepongeza juhudi za
Jumuiya ya Wazazi kata ya Ndala kwa kuonyesha mfano wa kuigwa katika kutatua
changamoto za jamii.
Katika hotuba yake, Diwani wa kata
ya Ndala ambaye pia ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mh.
Zamda Shabani, ameishukuru Jumuiya hiyo kwa juhudi zao za kuleta maendeleo.
Amesisitiza umuhimu wa kushirikiana
katika kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye mazingira salama na yenye maadili
mema.