Na Mapuli Kitina Misalaba
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Mhe. Ally
Hapi, amempongeza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi,
kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo, hali ambayo amesema
imejenga imani ya wananchi kwa Chama na kuhakikisha ushindi wa CCM kwenye
uchaguzi mkuu.
Hapi amehimiza wabunge na madiwani kuendelea kuchapa
kazi na kukamilisha ahadi walizotoa kwa wananchi badala ya kuvunjika moyo na
wanaotamani nafasi zao.
Hapi pia amesisitiza udhibiti wa nidhamu kwa
wanachama wanaoendesha kampeni kabla ya wakati ambapo ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha
wale wanaoanza kutangaza nia mapema dhidi ya kushirikiana na madalali wa
kisiasa, akisema, “Watiania jihadharini na wapambe feki; siasa ni kama ulevi,
mtauza kila kitu na kubaki weupe.”
Aidha, Hapi amesema uchaguzi huu ni wa kujipanga kwa
kila mgombea kubebwa na kazi alizofanya badala ya kupanga safu za wajumbe,
akibainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa mwongozo wa kuhakikisha
nidhamu inazingatiwa na kwamba TAKUKURU
itasimamia uchaguzi ndani ya Chama ili kuhakikisha haki na maadili
yanazingatiwa.
Hapi ametoa wito kwa viongozi wa CCM na wagombea
kuhakikisha wanatumia kampeni kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ili kupata ushindi wa kishindo kupitia siasa za kisayansi na hoja
madhubuti.
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi, amesoma taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2024, akidai kufanikisha
utekelezaji kwa asilimia 100.
Mhe. Katambi,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu
Wenye Ulemavu), ameainisha mafanikio katika sekta mbalimbali, zikiwemo elimu,
afya, maji, miundombinu, nishati safi ya kupikia, michezo, na ujenzi wa chama.
ELIMU
Amesema katika
kipindi chake shule mpya tisa zimejengwa
zikiwemo za msingi tano na sekondari nne
ambapo pia amefanikisha kuanzishwa kwa tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo na upanuzi wa Chuo Kikuu cha Moshi (MUCOPS) tawi la Kizumbi.
MIUNDOMBINU
Katika
kipindi chake, barabara na madaraja korofi kama Uzogole, Iwelyangula,
Kitangili, Ndala, na Mwamalili yameboreshwa ambapo ujenzi wa stendi mpya na
ukarabati wa masoko kama Ngokolo Mitumbani, Ibinzamata, na Kambarage
umefanikishwa.
AFYA
Katambi
amesema amejenga zahanati sita na kuboresha vituo vya afya, kikiwemo Kituo cha
Afya Kambarage ambapo zaidi ya ambulansi sita zimepokelewa kwa msaada wa Rais
Samia Suluhu Hassan.
MAJI
Amesema
jimbo hilo limepokea shilingi bilioni 195 kwa ajili ya usambazaji wa maji
katika maeneo mbalimbali, na utekelezaji utaanza mwaka wa fedha 2024/2025.
MICHEZO
Katambi
amezindua ligi mbalimbali kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana, huku zawadi
kwa washindi zikifikia hadi shilingi milioni 6.
UJENZI WA
CHAMA
Amesema
amejenga ofisi za CCM, ikiwemo ofisi ya Ibadakuli kwa gharama ya milioni 54 na
ya Chibe kwa milioni 48.
Mbunge Katambi pamoja na mambo mengine amekabidhi
vifaa mbalimbali kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kiti mwendo kwa mtoto mwenye
ulemavu Delfina Mashaka. Katibu Mkuu Hapi alikabidhi kiti hicho pamoja na spika
nne na maikrofoni nne kwa uongozi wa Stendi ya Mabasi ya Mkoani, ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Katambi kwa wananchi.
Katibu wa
CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, amempongeza Katambi kwa utekelezaji
mzuri wa ilani ya CCM na kuonya wanachama wanaofanya kampeni kabla ya wakati.
Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ally Hapi akizungumza.
Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Chama Mapinduzi (CCM) Ally Hapi akizungumza.Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini 2020/2024Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Paschal Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akizungumza.