Na Elisha Petro
Katibu wa tawi la Yanga SC Shinyanga Mjini na Katibu wa klabu ya Majengo Stars ndugu Juma Matongo amefariki Dunia alfajiri ya leo tarehe 15.1.2025 akiwa anaendelea na matibabu katika hospital ya Bugando Jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga Bwn. Sylivester Budete amethibitisha kupokea taarifa ya kifo hicho na kubainisha kuwa marehemu (Juma Matongo) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu kwa muda mrefu.
Misalaba Media inaungana na ndugu,jamaa na marafiki wote kutoa pole kwa viongozi wa michezo Mkoa wa Shinyanga,viongozi wa tawi la Yanga SC Shinyanga Mjini na wanamichezo wote Kwa taarifa ya majonzi "RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIA APUMZIKE KWA AMANI AMINA"