Apostle Samweli kisinza Ambaye pia ni mchungaji wa Kanisa la Uzima Tele Mkoani Mwanza amewataka waumini wa kanisa Hilo kumwamini Mungu na Kuyashika Mafundisho ambayo amekuwa akiyatoa.
Akizungumza katika Ibada ya tarehe 5/1/2025/Mwanzoni mwa Mwaka alisema ni wajibu wa Kila Muumini kumwabudu Mungu na Kuyashika Yale yanayofundishwa na Watumishi wa Mungu
Kisinza ameelezea mambo matano ya Kuyashika Mwanzoni mwa Mwaka Ikiwa ni Kuhakikisha Wanashikamana na Madhabui Ili hata unapokuwa unakutana na Changamoto Madhabahu yatakutetea.
Mchungaji huyo alisema watu wengi wamekuwa wakipitia wakati Mgumu Kwa Sababu ya Maneno waliyo yatamka wenyewe hivyo ni vyema kujitamkia Neno Jema Kwa Sababu Neno ni Uhai ukilitamka Linaumbika.
Alizungumza maneno hayo Kwa kutumia vifungu Mbali Mbali vyilivyopo kwenye Biblia.