Na Mapuli Kitina Misalaba
Baadhi ya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga wamezungumzia changamoto kubwa zinazowakabili wananchi katika maeneo
yao, hususan katika sekta za miundombinu ya barabara, elimu, na afya.
Kauli hizo zimetolewa leo kwenye kikao cha baraza la
madiwani cha robo ya pili kilicholenga kujadili taarifa za kata ambapo wamesema
kuwa ni muhimu kutengewa bajeti maalum ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa
kwa uharaka.
Katika kikao hicho, madiwani wamekubaliana juu ya umuhimu wa kushughulikia matatizo yanayohitaji majibu haraka, na pia wameelezea kuridhishwa kwao na juhudi zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali katika kutatua baadhi ya changamoto.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. Francis Philip ameelezea matumaini yake kuwa changamoto zote zilizotolewa na madiwani zitapewa
majibu mwishoni mwa robo hii na kuingizwa kwenye bajeti zinazofuata ambapo
amewasisitiza wakuu wa idara kuhakikisha
wanachukua hatua madhubuti kwa kutekeleza maombi ya madiwani.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu Emmanuel Jonhson amekiri kupokea changamoto hizo na kusema kuwa zitaingizwa kwenye
bajeti ili kutatuliwa ambapo amesisitiza umuhimu wa maafisa mipango kuhakikisha
changamoto hizo zinashughulikiwa kupitia bajeti inayohusika.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu Mhe. Francis Philip Manyanda wakati akisisitiza changamoto
hizo kushughulikiwa.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. Francis Philip Manyanda akifunga kikeo cha leo Januari 28, 2025.