Na Mwandishi Wetu Shinyanga.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Shinyanga mbele ya
Hakimu Mkazi Catherine Langau imetupilia mbali Maombi ya wadaiTushikamane
Gold Mine Group dhidi ya wadaiwa ambao ni Kampui ya Kichina ya TIAMPIN
Investment Company Limited na wenzao kwenye kesi ndogo yaliyotokana na kesi ya
msingi namba 9/2023.
Katika Madai hayo Januari 15, 2025, wakili wa wadai
Paul Kaunda aliiomba Mahakama ifute ushahidi wote uliowahi kutolewa na upande
wa wadaiwa kwani walishindwa kujibu Maswali ya wadai kwa kiapo na wa muda
kama inavyotakiwa kisheria.
Januari 20, 2025 Pande zote mbili zilifika
mahakamani, pamoja na mambo mengine mahakama ilikuwa kimya kusubiri Hakimu
afike ili kusikiliza maamuzi ya kama ushahidi utafutwa ili kesi
isikilizwe upande mmoja ambapo muda mfupi baadae Hakimu alifika, na
wakili Paul Kaunda anayewatetea wachimbaji wadogo katika mgodi uliopo kata ya
Mwakitolyo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ‘Tushikamane Gold Mine Group’
akaanza hivi;
"Mheshimiwa Ikupendeze naitwa wakili Paul
Kaunda ninayewawakilisha wadai zaidi ya 20 na upande wa pili yupo wakili Shaban
Mvungi anayewatetea wadaiwa tuko tayari kusikiliza uamzi kama ilivyorekodiwa na
mahakama hii Januari 15, 2025.
Baada ya Wakili Mvungi kusema yuko tayari kusikiliza
uamuzi, Hakimu alianza kusoma uamuzi wa kesi hiyo ndogo na kupinga baadhi ya
Maswali yaliyoelekezwa kwa wadaiwa kwa alichosema kuwa Maswali hayo
hayaendani hivyo yasijibiwe, na akataja maswali ambayo alidai yajibiwe na
wadaiwa kuwa ni namba 2,4,5,6,7 na 8
Baada ya amri hiyo ya mahakama, wakili Kaunda
akaiomba mahakama kuwa Maombi yaliyoletwa na mjibu Maombi namba tatu John
Mpimi yafutwe chini ya amri ya 1 kanuni ya 12, kwa kukiuka maaharti ya
lazima.
"Hicho kiapo kilicholetwa na John Kidimi
kifutwe kwa sababau kimekiuka masharti ya lazima ya amri ya 1 kanuni ya 12 ya
sheria ya Mwenendo ya mashauri ya madai sura namba 33" alisema huku
akiomba kuisoma kwa maslahi mapana ya haki.
"Kama kuna mdaiwa zaidi ya mmoja, mmojawao
anawwza kuchaguliwa kuwawakilisha wengine, akaapa kwa niaba ya hao wengine,
sasa katika kiapo cha
Bwana John Kidimi ambaye ni mjibu Maombi namba 3,
katika aya ya pili ya kiapo chake anasema hivi"
"Nimeruhusiwa na wajibu maombi wengine watano
TIAMPIN Investment Co Limited, Tushikamane old Mine Group, Tabu Lukanda, Alfred
Obama na Masinde Mabula kuapa kwa niaba yao"
" Watuletee barua inayoonyesha kuwa John Kidimi
alipewa idhini na wadaiwa hao, kwa hiyo waandae barua inayoonyesha kuwa John
Kidimi amepewa ruhusa na wahusika na ruhusa hiyo isajiliwe Mahakamani na
kupokelewa" alilalamika Kaunda.
" Nyalaka ya kutoka kwa kina TIAMPIN ambayo inampa
nguvu ya Kuapa kwa niaba yao haipo, labda nyie mahakama ipo kwenye kumbukumbu
zenu, na kama haipo chochote ambacho kimefanyika kwenye hizi nyalaka ni batili
na hakistahili kuwepo mahakamani" alisisitiza Kaunda."
Alisema kama hitaji hilo limekamilishwa wakili wao
aonyeshe ukamilifu wa matakwa ya kisheria kwa kuonyesha namba ya malipo na
namna alivyoshughurikia takwa hilo.
" Nisisitize mheshimiwa, Lugha ya sheria ambayo
imetungwa na Bunge letu hicho Kifungu kidogo cha 2,
hiyo nyalaka inaendana na barua ya watoa idhini,
sasa kama haipo na Lugha hapa ni 'Shall' hakistahili, na hatari ya kukosa
idhini hiyo....
Hakimu; wewe wakili nimeshatoa maamuzi tena
unanirudisha nyuma, unaona unachokifanya?
Wakili Kaunda; mimi siko huko, nauliza kitu ambacho
ni contraven lakini sio huko.
Hakimu; Unapoteza muda tu.
Wakili Kaunda; Sipotezi Muda, mimi najua
ninachokifanya, kama mheshimiwa utasema tunapoteza muda mbele ya hadhira hii ni
ajabu sana.
Wakili Kaunda; Acha niwasilishe halafu upande
wa pili naye awasulishe halafu uipige chini hapa.
Hakimu: sasa unavofanya unarudisha mambo nyuma na
ungeenda mbele tusipoteze muda.
Wakili Kaunda; sasa ukisema hivyo mimi nawakilisha
wateja wangu hawa utaelewekaje? alihoji huku akifunga begi lake, ishara ya
kuondoka.
Hakimu; Mimi nimeshajua malengo yako, kwenye suala
la kuwa kuna kiapo au hakipo si nimetoa uamuzi kule nyuma?alihoji.
Wakili Kaunda; Wapi Mheshimiwa, kwenye amri ya
kwanza ni wapi, sema tu tuondoe.
Baadae Hakimu alimruhusu wakili Mvungi
achangie kabla kumuonya shabidi Daniel Mapunda aliyefika kwa wito
wa mahakama ili kutoa ushahidi upande wa Wachimbaji wadogo wa Tupendane Gold
Mine.
Hakimu Catherine aliahirisha shauli hilo hadi Januari 28 litakapokuja kwaajili ya kuendelea.