MBUNGE SAGINI AFUNGUA MWAKA MPYA 2025 KWA KUWAPONGEZA WENYEVITI WA VIJIJI NA VIONGOZI WA MATAWI CCM KWA USHINDI WA ASILIMIA 98.1


Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Jumanne  Sagini amekutana na Wenyeviti wa Vijiji na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya matawi na baadhi ya mabalozi Wilaya ya Butiama kuwapongeza kwa ushindi wa asilimia 98.1 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na Viongozi hao katika hafla hiyo iliofanyika nyumbani kwake Kijijini Kiabakari Kata ya Kukirango leo Januari 01, 2024 Sagini amesema kuwa CCM ilishinda kwa kishindo uchaguzi uliopita kutokana na miradi ya mbalimbali ya kimaendeleo iliyopo katika jimbo lake.

"Wananchi wamekuwa na utulivu katika upigaji kura kwa kutazama miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita yenye Kauli mbiu yake ya Kazi Iendelee inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo kazi ya ilikuwa ndogo na wapiga wwnanchi walichukua na kuweka waa bila kuwa na mashaka," amesema Mhe. Sagini.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Butiama Christopher Siagi amewataka viongozi hao kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kutopoteza uaminifu kwa wananchi waliowaamini mpaka kuwapa ushindi wa kishindo.

Pia Siagi ametumia fursa hiyo kuwapiga marufuku baadhi ya viongozi wa chama wanaojikusanya kwa watu ambao wanahitaji nafasi za ubunge na udiwani ndani ya chama katika uchaguzi ujao.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Butiama, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Butiama, viongozi wa Dini, Serikali, Vyama rafiki, Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Viti Vitano Bara Ndg. Mariam Sagini na Viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka Kata zote 18.





Previous Post Next Post