WAKILI Sophia Tarimu akimsikiliza mchungaji Simon Hano katika zoezi la kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika uwanja wa Sokoine wilayani Igunga mkoani Tabora.
Na Lucas Raphael,Tabora
Wakati Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inaendelea kufanyika maeneo mbalimbali nchini , Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora , kampeni hiyo imebaini kuwa watu wengi wanakabiliwa na changamoto ya Migogoro ya ardhi , Miradhi na ndoa ambapo wanaume wengi wamekuwa wakitelekeza familia zao na kuanzisha familia zingine (nyumba ndogo)
Akizungumza na Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora Grace Mwema wakati wa utoaji wa huduma hiyo wilayani humo iliyofanyika leo katika uwanja wa Sokoine wilayani humo.
Alisema kwamba migogoro hiyo inapaswa hasa ya ndoa imewaacha vibaya kina mama wengi wakiwa na maumivu makubwa kwani wameachiwa watoto na kuwalea wenyewe bila ya kupata msaada wa mumewe.
Alibainisha kuwa changamoto hizo zimekuwa zikiwakabili wananchi wengi huku wakiwa wahajui sehemu sahihi pa kuziripoti ili wapate msaada wa kisheria .
Kwa upande wake Wakili kutoka wizara ya Katiba na sheria Mwanaidi Msangi alifafanua kwamba mpaka sasa wamewafikia watu zaidi ya 300 Wilayani humo na kubaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali .
Hata hivyo alisema kwamba changamoto ambazo zinaitaji ufafanuzi zaidi wameziripoti kwenye ngazi zingine za juu za utoaji haki ikiwemo mahakamani.
Baadhi ya wakazi Wilayani humo Mashaka Bundala na Simon Hano, waliishukuru serikali kwa kupeleka Kampeni hiyo na kutaka iwe endelevu ili waweze kupata elimu ya Kisheria itakayokuwa mwarobaini wa migogoro yao .
Kampeni ya msaada kisheria wa Mama samia imelenga kuyafikia makundi mbalimbali ya Wananchi ili kutoa huduma na elimu ya masuala mbalimbali yanayohitaji Msaada wa kisheria .
Mwisho