Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkataba wa ujenzi wa miradi tisa ya maji kwa mwaka
wa fedha 2024/2025 umesainiwa katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkoa
wa Shinyanga, ikihusisha wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga,
Mhandisi Julieth Payovela, miradi hiyo inajumuisha miradi mitano katika Wilaya
ya Kishapu, miradi miwili katika Wilaya ya Kahama, na mradi mmoja katika Wilaya
ya Shinyanga.
Aidha, mkataba wa utekelezaji wa programu ya
uchimbaji wa visima 900 pia umesainiwa, ambapo kila jimbo katika mkoa wa
Shinyanga linatarajiwa kupata visima vitano.
Miradi yote hiyo, ambayo itagharimu zaidi ya
shilingi bilioni 4.7, inatarajiwa kunufaisha wakazi wa majimbo sita ya Mkoa wa
Shinyanga ambayo ni Shinyanga Mjini, Ushetu, Kahama, Kishapu, Msalala, na
Solwa.
Kampuni zitakazotekeleza miradi hiyo ni pamoja na Jonta
Investment Ursino Limited na MIWI Construction Co. LTD.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe Anamringi Macha, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika
utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa
viwango vinavyostahili.
Kwa niaba ya wakandarasi, Mnadi Mnadi ameahidi kuwa
miradi yote itatekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati ili kuwanufaisha
wananchi.
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali
wa serikali na chama, wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim Iddi
na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akizungumza
katika hafla hiyo leo Januari 24, 2024.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth
Payovela, akitoa taarifa ya miradi hiyo ambayo imesainiwa leo Januari 24, 2024.

Zoezi la utiaji
saini ya ujenzi wa miradi ya maji kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 likiendelea katika
ukumbi wa Mkoa wa Shinyanga na kwamba hafla hiyo imeshuhudiwa na viongozi
mbalimbali huku mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Zoezi la utiaji saini ya ujenzi wa miradi ya maji kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 likiendelea katika ukumbi wa Mkoa wa Shinyanga na kwamba hafla hiyo imeshuhudiwa na viongozi mbalimbali huku mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.
Picha ya pamoja viongozi mbalimbali na wakandarasi.