MKATABA WA MIRADI YA MAJI YENYE THAMANI YA BILIONI 4.7 WASAINIWA MKOANI SHINYANGA RC MACHA ATAKA WANANCHI WASHIRIKISHWE

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkataba wa ujenzi wa miradi tisa ya maji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umesainiwa katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkoa wa Shinyanga, ikihusisha wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, miradi hiyo inajumuisha miradi mitano katika Wilaya ya Kishapu, miradi miwili katika Wilaya ya Kahama, na mradi mmoja katika Wilaya ya Shinyanga.

Aidha, mkataba wa utekelezaji wa programu ya uchimbaji wa visima 900 pia umesainiwa, ambapo kila jimbo katika mkoa wa Shinyanga linatarajiwa kupata visima vitano.

Miradi yote hiyo, ambayo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.7, inatarajiwa kunufaisha wakazi wa majimbo sita ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni Shinyanga Mjini, Ushetu, Kahama, Kishapu, Msalala, na Solwa.

Kampuni zitakazotekeleza miradi hiyo ni pamoja na Jonta Investment Ursino Limited na MIWI Construction Co. LTD.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Anamringi Macha, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.

Kwa niaba ya wakandarasi, Mnadi Mnadi ameahidi kuwa miradi yote itatekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wananchi.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa serikali na chama, wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim Iddi na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani.

Miradi minane inatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2025, huku mkataba wa uchimbaji wa visima ukiwa na muda wa mwaka mmoja na kwamba miradi hiyo itatekelezwa chini ya usimamizi wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akizungumza katika hafla hiyo leo Januari 24, 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akizungumza katika hafla hiyo leo Januari 24, 2024.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, akitoa taarifa ya miradi hiyo ambayo imesainiwa leo Januari 24, 2024. 

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, akitoa taarifa ya miradi hiyo ambayo imesainiwa leo Januari 24, 2024. 

Mnadi Mnadi akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wengine ambapo ameahidi kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati.





 

Previous Post Next Post