MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA WAKILI JULIUS MTATIRO KESHO KUFANYA ZIARA SHYDC

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, kesho Jumanne tarehe 14.01.2025, atatembelea vijiji mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga (vijijini) kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wakili Mtatiro atatembelea vijiji vitatu vya Kata ya Usanda, Tarafa ya Samuye na kukutana na wananchi kwa njia ya mikutano ya hadhara, kupitia ziara yake iliyopewa jina la "Kijiji kwa kijiji na DC Mtatiro" .

Wakili Mtatiro atakutana na wananchi wa kijiji cha Shabuluba kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, ambapo kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 9:00 Alasiri atakutana na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ngaganulwa.

Mtatiro atahitimisha ziara yake kwa kukutana na wananchi wa kijiji cha Nzagaluba, kuanzia saa 9:30 Alasiti hadi saa 11:30 Jioni.

Previous Post Next Post