MWISHO WA SAFARI YANGU RADIO FARAJA FM, MWANZO MPYA KUPITIA MISALABA MEDIA

Baada ya kutumikia kwa moyo wa dhati kama Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Faraja FM kwa takribani miaka mitano, nimefikia hatua ya kuhitimisha rasmi safari yangu katika kituo hiki. Ukweli imekuwa safari ya kipekee ambayo sitaisahau.

Natoa shukrani za pekee kwa uongozi wa Radio Faraja FM kwa kuniamini, wafanyakazi wenzangu kwa mshikamano wa hali ya juu, na zaidi, ninyi wasikilizaji wetu waaminifu kwa upendo wenu na ushirikiano usio na kifani.

Safari hii imekuwa ya mafanikio makubwa kwangu, lakini sasa ninaelekeza nguvu zangu katika kuimarisha jukwaa langu la habari mtandaoni, MISALABA MEDIA. Hii ni hatua mpya, lakini nitaendelea kuwa sehemu ya maisha yenu kupitia habari na maudhui tofauti mtandaoni.

Huu ni mwisho wa safari yangu hapa, lakini sio mwisho wa uhusiano wetu. Naondoka nikiwa na moyo wa shukrani kwa kila mmoja wenu.

Nawaombea kila la heri, na naamini bado tutaendelea kuwasiliana kupitia MISALABA MEDIA.

Asanteni sana, na Mungu awabariki!

Previous Post Next Post