Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha,
amemuapisha Peter Nicholaus Masindi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, kufuatia
uteuzi wake wa hivi karibuni uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Hafla ya uapisho huo imefanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali, wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, RC Macha amemtaka
Masindi kuhakikisha Wilaya ya Kishapu inaendelea kuwa na amani na usalama huku
akisisitiza kushughulikia changamoto za wananchi kwa vitendo ili kuimarisha
maendeleo ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu,
Peter Masindi, ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kuzingatia
kanuni na miongozo iliyopo ambapo amesema lengo ni kuleta matokeo chanya katika
maendeleo ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na wadau wote.
Uteuzi wa Masindi ni sehemu ya juhudi za serikali
kuhakikisha kuwa viongozi wenye maadili wanateuliwa ili kuleta maendeleo na
kuimarisha ustawi wa jamii katika ngazi za wilaya.