Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha,
ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote mkoani Shinyanga
kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu utunzaji wa mazingira na matumizi ya
nishati safi.
Akizungumza leo katika zoezi la upandaji miti lililofanyika
katika Shule ya Msingi Mapinduzi A na B, Mhe. Macha ameagiza hatua kali
zichukuliwe kwa mifugo itakayoruhusiwa kula miti inayopandwa.
"Mifugo yote itakayoonekana inalishwa katika maeneo haya ambayo
tumepanda miti hatua kali zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na kukamata mifugo hiyo.
Pia, maeneo ambayo tumeamua kuotesha miti tuhakikishe kuwa hatua zinachukuliwa
za kutunza hiyo miti," amesema Mhe. Macha.
RC Macha amesema Shinyanga ina mpango wa kupanda
miti milioni moja na laki tano ambapo amezielekeza Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kila mmoja
anachukua hatua za kusimamia upandaji na utunzaji wa miti.
"Mpango huu ni lazima tuufanikishe. Natoa rai kwa Halmashauri zote sita
za Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kila mmoja anachukua hatua za kusimamia
upandaji na utunzaji wa miti," amesema RC Macha
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili
Julius Mtatiro, ameahidi kutekeleza maelekezo hayo kwa vitendo.
"Maelekezo ambayo Mkuu wa Mkoa umetupatia ya kuendeleza kampeni ya
upandaji miti, sisi Wakuu wa Wilaya tutayasimamia kwa umakini ili kuhakikisha
tunaboresha mazingira ya Shinyanga," amesema Mtatiro.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko, naye ameahidi kuhakikisha miti iliyopandwa inatunzwa
vizuri.
"Tutaendelea kuzingatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha miti hii
inastawi vizuri na kufanikisha lengo la kuboresha mazingira," alisema
Masumbuko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akipanda
mti ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akipanda
mti ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akipanda
mti ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha
akitoa maelekezo baada ya zoezi la upandaji miti leo Januari 27, 2025 katika shule
ya msingi Mapinduzi A na B zilizopo kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti leo Januari 27, 2025 katika shule ya msingi Mapinduzi A na B zilizopo kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko, akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti leo Januari 27, 2025 katika shule ya msingi Mapinduzi A na B zilizopo kata ya Ngokolo.
TAZAMA VIDEO