SIMBA SC YAICHAPA CS SFAXIEN 1-0 UGENINI

Timu ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya wenyeji CS Sfaxien katika mchezo wa kundi A Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa  January 5, 2024 katika Uwanja wa Olympique Hammadi – Agrebi mjini Rades nchini Tunisia.

Bao pekee la Simba SC limefungwa na kiungo mshambuliaji Muivory Coast Jean Charles Ahoua dakika ya 34.

Kwa ushindi huo Simba SC imefikisha pointi tisa sawa na CS Constantine ya Algeria yenye pointi tisa baada ya kupata ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi Bravos do Maequis ya Angola katika mchezo uliochezwa leo, huku CS Sfaxien ikishika mkia kwa kupoteza mechi nne.

Previous Post Next Post