TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA KIKANDA WA BARAZA LA VIWANJA VYA NDEGE AFRIKA MKOANI ARUSHA









Waziri wa Uchukuzi , Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusu mkutano huo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Christian Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo.

……………

Happy Lazaro, Arusha .

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa baraza la viwanja vya ndege Afrika (ACI) na maonesho ya wadau utakaofanyika April mwaka huu mkoani Arusha na kuambatana na mkutano wa 73 wa Bodi ya ACI Africa.

Akizungumza na waandishi wa hahari mkoani Arusha leo Waziri wa uchukuzi ,Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa ,fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hilo muhimu ilitokana na ushindi walioupata kufuatia utaratibu uliowekwa na ACI Afrika wa kushindanisha nchi wanachama kuwa mwenyeji wa mikutano yake ambayo kwa mwaka hufanyika mara mbili.

Amesema kuwa ,mkutano huo utawakutanisha washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi takribani 54 barani Afrika ambazo ni wanachama wa baraza hili la kimataifa .

Ameongeza kuwa,uenyeji wa mkutano huo ni mwendelezo wa mafanikio ya kimkakati yanayoendelea kupatikana kupitia viwanja vya ndege .

“Kama mtakumbuka mnamo mwezi Septemba 2024 mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania kupitia kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere ilipata tuzo ya mshindi wa kwanza kutoka baraza la viwanja vya ndege Afrika (ACI Afrika) kwa kuwa kiwanja chenye ubora wa usalama kwa mwaka 2024 kwa viwanja vya ndege vya Afrika vyenye miruko zaidi ya elfu 50”.amesema.

Prof. Mbarawa amesema kuwa, tuzo hiyo imelipa heshima Taifa katika ukanda wa Afrika na duniani kwa ujumla na kuthibitisha ubora wa viwango vya usalama vinavyotekelezwa katila viwanja vya ndege nchini.

Amesema kuwa , ACI Afrika ndicho chombo kikuu cha kimataifa kinachosimamia maslahi ya viwanja vua ndege vya Afrika na dhamira yake kuu ni kuendeleza maslahi ya pamoja ya viwanja vya ndege ,kukuza ubora wa kitaaluma,na kusaidia maendeleo endelevu ya sekta ya usafiri wa anga katika.bara zima la Afrika .

Ameongeza kuwa,mpaka kufikia Novemba 2024 ACI Afrika ilikuwa na zaidi ya wanachama 75 wa viwanja vya ndege wanaoendesha zaidi ya viwanja vya ndege 265 katika nchi 54 Afrika ,pamoja na washirika 59 wa kibiashara.

Amefafanua kuwa ,moja ya jukumu la ACI Afrika ni kuwakutanisha pamoja nchi wanachama wa baraza hilo kuwexa kujadili masuala mbalimbali ya kiuendeshaji na kitaaluma yanayohusu viwanja vya ndege ,na pia kuviwezesha viwanja vya ndege kukutana na wafanyabiashara ,wawekezaji na mashirika ya kimataifa ya ndege na kuweza kunadi fursa walizonazo katika viwanja vyao.

Prof.Mbarawa ameongeza kuwa ,jukumu lingine la ACI Afrika ni kuwakutanisha nchi wanachama ili kujadiliana juu ya changu zinazovikabili viwanja vya ndege na lengo likiwa ni kuhakikisha kunakuwepo na uendelevu, usalama na ufanisi katika usafiri wa anga sambamba na uzingatiaji wa masuala ya kimazingira katika viwanja vya ndege .

Aidha kauli mbiu ya mkutano huo ni”Katika kuelekea wakati ujao bora wa kijani:kutumia usafiri wa Anga endelevu na utalii kwa ustawi wa kiuchumi.”

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa viwanja vya ndege ,Abdul Mombokaleo amesema kuwa,katika mkutano huo wadau tatribani 400 wanatarajiwa kushiriki.katika mkutano wakiwemo wadau kutoka sekta ya anga na biashara kwa ujumla ambapo utakuwa ni.fursa kubwa ya kiuchumi kwa mkoa wa Afrika kwani watakuja wadau mbalimbali wa kimataifa.

Amesema kuwa, mkutano huo wa kimataifa una maslahi mapana kwa nchi,mafanikio yake yanategemea ushirikiano wa wadau mbalimbali.wakiwemo wizara,taasisi,na mashirika mbalimbali ya serikali na sekta bianfsi yakiwemo mashirika ya ndege,kampuni za utalii ,wafanyabiashara, wakandarasi na watoa huduma ambao kwa nafasi zao serikali inatarajia watashiriki katika kuwezesha kufanyika kwa mkutano huo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Christian Makonda aliyeambatana na Mhe. Mbarawa, ameshukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wizara hiyo kwa Kuiteua Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa, akiahidi usalama wa kutosha pamoja na huduma nzuri kwenye maeneo ya malazi na kumbi za mikutano kwa wageni wote kwa siku zote saba za kufanyika Mkutano huo.
Previous Post Next Post