Na. JSM
Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Penal Code)
Kifungu cha 319; Uchomaji wa mali kwa makusudi.
Mtu yeyote ambaye, kwa kunuwia na isivyokuwa halali anatia moto katika–
(a) Jengo lolote lile liwe limekamilika au bado ; au
(b) chombo chochote kile kiwe kimekamilika au bado; au
(c) lundiko lolote la mazao ya mboga, au la makaa ya mawe, madini au la kuni; au
(d) viwanda vya machimbo au matengenezo au zana za machimbo ya madini atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha
maisha.
_______
Kifungu cha 320; Kujaribu kuchoma
mali.
Mtu yeyote ambaye–
(a) anajaribu isivyokuwa halali kuwasha moto kitu chochote kilichorejewa katika kifungu cha 319; au
(b) kwa kunuwia na isivyokuwa halali anatia moto kwenye kitu chochote ambacho kipo karibu na kitu chochote ambacho kimerejewa katika kifungu cha 319 na kuna uwezekano wa kushika moto kutoka hapo, atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka kumi na nne.
______
Kifungu cha 321 - Kutia moto katika mazao na mimea iotayo
Mtu yeyote ambaye kwa kunuwia na isivyokuwa halali anatia moto –
(a) mazao ya mavuno ya ukulima, yawe mitini, yamechumwa au yamekatwa; au
(b) mazao ya nyasi za kulisha wanyama zilizolimwa, ziwe za kuota zenyewe au za mazao ya asili ya ardhi hiyo au sivyo,
ziwe zimesimama au zimekatwa; atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka kumi na nne.
______
Kifungu cha 322 - Kujaribu kutia moto
mazao n.k.
322. Mtu yeyote ambaye–
(a) anajaribu isivyokuwa halali kuwasha moto kitu chochote kama kilichotajwa kwenye kifungu cha 321; au
(b) kwa kunuwia na isivyokuwa halali anatia moto kitu chochote kilichopo mahali ambapo kitu chochote kilichorejewa katika kifungu cha 321 kina uwezekano wa kushika moto kutoka hapo; atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa kifungo cha miaka saba.