VIJANA 200 WAFAIDIKA NA UFADHILI WA MASOMO KUPITIA MBUNGE CHEREHANI


Jumla ya Vijana 200 waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ndoa na mimba za utotoni na changamoto za kifamilia wamepata ufadhili wa kuendelea na masomo kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu katika Chuo cha Maendeleo Msaginya FDC mkoani Katavi.


Akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga Vijana hao, Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Emmanuel Cherehani, amewaasaa kuitumia vyema fursa hiyo ikiwemo kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu katika kipindi chote watakapokuwa masomoni.


Katika hatua nyingine, Cherehani amesema katika kipindi chote cha utawala wake ameendelea kufadhili masomo ya Wanafunzi mbalimbali wakiwemo wa elimu ya juu.


Kwa upande wake Mratibu wa elimu kata ya Nyamilangano, alipozungumza hafla hiyo, Kote Chacha aliwasisitiza kuwa waadilifu huku baadhi ya Wazazi na Wanafunzi hao wakimshukuru Mbunge Cherehani kwa fursa hiyo adhimu.


Hatua hiyo inalenga vijana hao kufikia ndoto zao kupitia fani mbalimbali ambapo kati yao Wasichana ni 150 na Wavulana 50.



Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza.















Previous Post Next Post