WABUNGE SHINYANGA WAIMWAGIA SIFA RUWASA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla hiyo.

Na Moshi Ndugulile, Misalaba Media

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka wananchi Mkoani Shinyanga kuwa wazalendo  katika jukumu la kutunza miradi ya maji inayowekezwa na serikali,  badala ya kuhujumu miundombinu hiyo, kwani kwa kufanya hivyo ni kuitia hasara serikali.

Ameyasema hayo kwenye hafla ya utiaji saini mikataba tisa ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ,kati ya RUWASA na wakandarasi wanaotekeleza miradi  hiyo ya maji.

RC Macha amesema serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake wa kujenga na kuboresha  miundombinu ya maji katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha upatianaji wa huduma hiyo,hivyo wananchi wanapaswa kutunza rasilimali hizo.

RC Macha ameiagiza RUWASA kutoa taarifa ya utekelezaji wa mradi kila tarehe 15 ya mwezi ili serikali iweze kujua maendeleo ya miradi hiyo,ikiwa ni hatua ya kuepuka kukwama kwa utekelezaji huo

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, amesema Miradi hiyo itajengwa katika Wilaya za  Kahama, Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na kwamba ujenzi wa miradi hiyo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita.

Mhandisi Payovela amefafanua kuwa, katika utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Shinyanga, vijiji vingi sasa vimepata huduma ya maji, na kwamba serikali imeongeza fedha za ujenzi wa visima 20 vya maji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kumaliza changamoto ya ukosefu wa maji.

Akizungumza katika hafla hiyo mbunge wa jimbo la Msalala wilayani kahama Mhe. Idd kassim ameipongeza serikali chini ya jemedari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kutekeleza miradi hiyo ikiwa ni juhudi zilizolenga kuondoa changamoto za kijamii kwa wananchi

“ tunakupongeza sana mheshimiwa mkuu wa Mkoa, wewe  pamoja na timu yako,kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kwenye mkoa wetu wa Shinyanga, ambayo mmeendelea kuifanya, nitakuwa mchoyo wa fadhila pia kama nisipomshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan,Mama na Rais wetu,kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kuifanya ya kutuletea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji kwenye majimbo yetu, Mimi mbunge wa jimbo la Msalala nimekuwa shuhuda wa miradi mikubwa ya maji ambayo Dkt Saia Suluhu Hassan ndani ya miaka mine,tunaenda mwaka wa tano sasa, imetekelezwa katika jimbo la Msalala,ambapo tunayo miradi mikubwa kadha wa kadha uiwemo mradi unaotoka Mangu-Ilogi,ambao umekamilika,lakini tuna mradi mwingine wa Busangi-Ntobo ambao umekamilika kwa gharama ya shilingi Bil.11,lakini ipo miradi inayoendelea kutekelezwa ukiwemo ule wa kanda ya Mwalugulu,kanda ya Jana na kanda ya Mwamkima na maeneo mengine.

Lakini tuna fedha nyingine ambazo Rais Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan ametupatia kwa ajili ya usambazaji wa maji kwenye kata ya Bugarama na Bulyanhulu ambao tayari umekamilika na wananchi wananufaika na huduma ya maji ya ziwa Victoria”ameeleza Mbunge Idd Kassim

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe. Emanuel Cherehani ameipongeza  RUWASA ambayo ameitaja kuwa imeendelea kutatua changamoto ya maji kupitia miradi mbalimbali  iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa

Ameomba kila mdau wa maji  atambue wajibu wa kudhibiti upotevu wa maji na kwamba iwe ni kipaumbele cha kushughulikia,ambapo amewataka wakandarasi wanaopewa kazi hiyo kuhakikisha vifaa vyao vinakuwa imara na vyenye ubora wenye kiwango

Hafla ya utiaji saini mikataba tisa ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kati ya RUWASA na wakandarasi wanaotekeleza miradi  hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali na Chama tawala CCM, wabunge,wakuu wa wilaya,kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa.

Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) itaanza utekelezaji wa  ujenzi wa miradi tisa ya maji   yenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni 4.7 utakaonufaisha vijiji 16 katika wilala za Kishapu,Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga

MWISHOMeneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela.Mbunge wa jimbo la Msalala wilayani kahama Mhe. Idd kassim akizungumza.Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe. Emanuel Cherehani akizungumza.

Previous Post Next Post