WANAFUNZI URAMBO WALALAMIKIA WALIMU KUWACHAPA VIBOKO KUPITILIZA

Na Lucas Raphael, Misalaba MediaTabora 

 

WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari wilayani Urambo mkoani Tabora wamewalalamikia walimu wao Kwa kuendeleza vitendo vya kikatili kwa kuwachapa  viboko sehemu mbalimbali za mwili wakati ni kinyume na utaratibu wa wizara ya elimu Tanzania.

 

Kauli hiyo iliotolewa na wanafunzi hao  mbele ya timu iliyoendesha zoezi la kampeni ya msaada wa kisheria ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika shule ya sekondari Matwiga wilayani Urambo mkoani Tabora .

 

Wanafunzi hao wa shule ya sekondari Matwiga iliyopo kataya itundu wilayani humo  John Kilisa ,Agnes Madaraka na Pili Ramadhani kwa niamba ya wanafunzi wenzao walisema kwamba walimu wamekuwa wakiwachapa vikobo bila kujali wapi pa kuchapa .

 

Walisema kwamba walimu wengini wanachapa kiboko vilivyodia idadi hali inayopelekea wanafunzi kuona shule kama nisehemu ya mateso na sio kujifunza .

 

Waliendelea kubainisha kwamba walimu wanachapa migogoni ,mabegani matakoni na mikono  hivyo vyote vinaonsha vitendo vya kikaliti kwa watoto wa shule .

 

Hata hivyo mratibu wa kampeni hiyo kutoka wizara ya katiba na sheria wilaya ya Urambo mkoani hapa Dkt Baraka Mkami aliwataka walimu  wilayani humo  kufuata kanuni na tararibu za uchapaji wa viboko kutoka wizara ya Elimu na kuacha kuvunja sheria elekezi .

 

Alisema kwamba vitendo vya kikatili vipo vya aina nyingi ikiwemo kucha viboko vilivyopitiliza hivyo ni muhumu kurudi kwenye maadali ya ualimu kwa kuafuara taratibu zinavyosema.

 

Naye mkurungezi wa shirika lisilo la kiserikali la Urambo Legal Availment Ada Charity (ULAC) Alfered Kalugendo alisema walimu wanapaswa kuchapa viboko visivyodia 4 tu kwa mwafanzi na si vinginevyo .

 

Hata hivyo aliwataka walimu kuacha kuwachapo viboko hovyo wanafunzi kwa kufanya hivyo kunapunguza morali ya wanafunzi kusoma na kujifunza na hivyo kunawajenga wanafunzi kuwa na hofu kutoka kwa walimu baadhi na siyo wengine .

 

Aidha Dkt Mkami alisema kwamba wameshatembea shule 10 za msingi 6 na sekondari 4 na wamekutana na zaidi ya watu 5000 kutoka katika kata tano walizotembea hadi kufikia leo na wanaendelea ili kudhirisha na malalamilo hayo.

 

 Mwisho

 


 

Previous Post Next Post