WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA KUHUSU KILIMO

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2025 ameshiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda.


Awali Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia Tamasha la Kahawa Afrika (Africa Coffee Festival) lililolenga kuhamasisha uongezaji thamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa.

Previous Post Next Post