WAZIRI MWITA : SERIKALI IMEJENGA MIUNDOMBINU YA KUHIFADHI MAZAO YA CHAKULA











Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akikata utepe, kuashiria Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka huko Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka huko Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid akitoa salamu za Wananchi wa Mkoa huo katika Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka,Ufunguzi ambao umefanyika Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Ali Khamis Juma akitoa taarifa ya kitaalamu katika Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka huko Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka huko Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Muonekano wa Ghala jipya la kisasa la kuhifadhia nafaka, lililopo Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

………..

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Serikali imejenga Miundombinu ya kuhifadhi mazao ya chakula ili kupata uhakika wa Chakula Nchini.

Amesema Majengo hayo yatasaidia kulinda afya ya jamii na kuimarisha biashara ya mazao ambayo yatahifadhi nafaka na kuwa katika hali ya Usalama.

Ameyasema hayo katika Ufunguzi wa Ghala la kuhifadhia nafaka huko Ole Dodeani Wilaya ya Chake chake, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amebainisha kuwa kutokana na matatizo yanayoweza kujitokeza kwa kula chakula kilichokuwa si salama Serikali imelipa kipaumbele suala la Usalama wa Chakula.

Aidha amesema Ghala hilo ni muhimu kwani litaweza kuhifadhi Nafaka na chakula kuwa katika hali ya Usalama.

Mbali na hayo amesema Ghala hilo pia litasaidia Biashara ya Utalii, kuimarika na kukuza Uchumi wa Nchi kwani Wageni wanaoingia Nchini watakuwa na Imani ya kula Chakula salama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaunganisha Wananchi katika Kilimo jambo ambalo limeonyesha jinsi anavyowapenda Wananchi wake.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Ali Khamis Juma amesema mradi huo, umekusudia kudhibiti Magonjwa yatokayao na Sumu kuvu hasa kwa Mazao ya Nafaka.

Aidha amesema Wizara inaendelea kuimarisha Miundombinu ikiwemo ya Ujenzi wa Maghala mapya na Ukarabati wa Maghala Makongwe.

Ghala hilo limejengwa na Serikali kupitia mradi wa kuhifadhi Sumu kuvu Tanzania na umeanza mwaka 2019 na unatarajiwa kumalizika mwezi mei mwaka huu ambapo umefadhiliwa na Programu ya uhakika wa Chakula na lishe chini ya Bank ya Dunia Pamoja Banki ya Afrika (ADB).
Previous Post Next Post