Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Uongozi wa Wizara ya Maji umeridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe.
Ukaguzi wa mradi huo umefanyika na timu ya Menejimenti ya Wizara ya Maji ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri.
Mhandisi Mwajuma amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe wanaondokana na adha ya huduma ya maji.
Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji itahakikisha inaendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ikiwemo matumizi ya Dira za malipo kabla ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe . Dkt. Samia Suluhu Hassan.hivyo wananchi wa Same Mwanga wategemee matokea makubwa na mazuri.