Na.Belnardo Costantine, Misalaba Media
Tukio la kushangaza limetokea Dodoma Magorofani Ihumwa ambapo kijana mmoja alijifanya msicha VPna na kupata ajira ya house girl katika familia ya askari. Kijana huyo Ambaye jina lake halisi halijafahamika alijificha kwa kuzingatia mavazi ya kike na alijifanya kuwa msichana ili kumsaidia mke wa askari, ambaye alikuwa mjamzito, bila ya kujua kwamba house girl huyo ni mwanaume. Aliishi katika familia hiyo kwa muda mrefu bila kugundulika.
Kijana huyo aligundulika baada ya mke wa askari kugundua ishara za mwili kupitia mikono ya house girl, ambazo zilionyesha kuwa si za kike. Alitoa taarifa na uchunguzi ulifanywa, na kugundulika kwamba house girl alikuwa kijana wa kiume aliyejivisha mavazi ya kike. Mtuhumiwa alikamatwa na kukabidhiwa kituo cha polisi cha Ihumwa.
Post a Comment