" BODABODA WA UHALIFU WA KUTUMIA PIKIPIKI ISIYO NA NAMBA ZA USAJILI."KISHANDU" ADAKWA

BODABODA WA UHALIFU WA KUTUMIA PIKIPIKI ISIYO NA NAMBA ZA USAJILI."KISHANDU" ADAKWA


Na Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa ufafanuzi kuhusiana na ‘video’ inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio la lililofanywa na askari polisi wakati wa ukamataji Kwa mwendesha bodaboda  ambaye ametambulika kwa jina la Rajabu Hassan lililotokea katika eneo la Maili Moja mkoani Pwani, kuwa ni mtuhumiwa wa siku nyingi aliyekuwa akiwakimbia askari waliokuwa wakijaribu kumkamata baada ya kufanya uhalifu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rajabu alikuwa anatafutwa na polisi kutokana na tuhuma mbalimbali za kujihusisha na matukio ya uporaji kwa kutumia pikipiki ikiwa imekunjwa namba za usajili (plate number) na wakati mwingine anatumia pikipiki ambayo haina namba ya usajili maarufu vishandu.
 hatahivyo wakati wa tukio hilo la kumkamata, pikipiki aliyokuwa anatumia kuwakimbia Askari haikuwa na namba ya usajili.
"Baada ya kufikiwa na askari Rajabu alianzisha vurugu za kukaidi kukamatwa licha ya Polisi kujitambulisha kwake, hata hivyo walimkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Kibaha ili kuendelea na taratibu zingine za kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili."Taarifa ya polisi
 

Post a Comment

Previous Post Next Post