" CCM IMEJIPANGA KUSHIKA DOLA

CCM IMEJIPANGA KUSHIKA DOLA


Na Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Spika wa Bunge jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt.Tulia Acksoni .
 amesema chama cha mapinduzi "CCM" imejipanga kuhakikisha kinaendelea kushika dola katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa kuwa kazi iliyofanywa na Serikali inatosha kutangaza sera za ushindi.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Leo tarehe 20 mwezi wapili mwaka huu, akizungumza na wanachama wa CCM katika Ukumbi wa CCM Hanyegwamchana baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kusini Unguja 

Hata hivyo Dkt. Tulia amewataka vijana wa CCM wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kujitokeza kwa wingi ili waweze kuonesha uwezo wao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa..



Post a Comment

Previous Post Next Post