" DKT. SLAA YUKO HURU.

DKT. SLAA YUKO HURU.


Na Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Dk. Wilbroad Slaa (76) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DDP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Dk. Slaa mwanasiasa mkongwe alikabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani ukifahamika kama Twitter), kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao.

Dk. Slaa ameachiwa huru mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga, kesi hiyo ilipoletwa Mahakamani. Hakimu Kiswaga alisema kuwa kesi hiyo ina pande mbili, ambazo ni maombi yaliyowasilishwa na upande wa jamhuri pamoja na kesi ya msingi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema, akisaidiana na Wakili Clemence Kato, walidai kuwa maombi yaliyowasilishwa na upande wa jamhuri ya kupinga dhamana ya mshitakiwa yaondolewe.

"Tunaomba hili liingie kwenye kumbukumbu za Mahakama kuwa tunaomba kuondoa maombi tuliyowasilisha upande wa mashtaka la kupinga dhamana ya mshitakiwa Slaa," alidai Mrema.



Post a Comment

Previous Post Next Post