Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, ameshiriki katika clinic ya Samia Teacher's Mobile Clinic iliyofanyika Mkoani Geita. Clinic hii inaendeshwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kwa kushirikiana na ofisi mbalimbali za serikali ikiwemo Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na Tume ya Utumishi wa Walimu. 

Lengo kuu la clinic hii ni kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba walimu.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, ambaye ametoa hotuba kuhusu umuhimu wa juhudi za pamoja katika kuboresha hali ya walimu nchini.