MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, ameendelea kuwamwagiwa sifa kede kede juu ya uletaji wa maendeleo kwa kila Kata Jimboni kwake.
Katambi jana amefanya ziara katika Kata ya Chamaguha pamoja na Ndembezi,kwa kukutana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kwa Kata hizo, pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara kuwaeleza yale ambayo ameyatekeleza kwao ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge.
Diwani wa Ndembezi Victory Mmanywa, amemwagia sifa Katambi, kwamba ni Mbunge ambaye ana kasi kubwa ya maendeleo ambapo Kata hiyo ndani ya miaka Minne ya Mbunge Katambi imepiga hatua kubwa kimaendeleo tofuati na ilivyokuwa awali.
Amesema kwenye Kata hiyo kulikuwa na ujenzi wa Machinjio ya kisasa ambayo ilishindikana kukamilika,lakini alivyoingia Katambi kwenye Ubunge aliipambania na kuikamilisha na sasa inatoa huduma ya kuchinja mifugo.
Amesema mbali na machinjio hiyo, pia kwenye Kata hiyo zimejengwa shule mbili mpya za Sekondari, ikiwamo ya Butengwa, pamoja na shule ya wasichana wenye vipaji maalumu.
“Katambi ni Mbunge mwenye kasi kubwa ya maendeleo Ndembezi haikuwa hivi imepiga hatua kubwa kimaendeleo, nilikuwa nikimpigia simu mheshimiwa Ndembezi kuna hitajika hiki ana niahidi kuwa atashughulikia na muda mfupi kwenye unaona matokeo,”amesema Mmanywa.
Ameongeza, kulikuwa pia kuna madaraja ambayo yalishindikana kujengwa tangu enzi za ukoloni likiwamo la Mwanoni, lakini kwenye Utawala wa Katambi, daraja hilo limejengwa pamoja na kulijenga upya tena daraja la Mazinge.
Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga, amemwangia sifa Katambi, kwamba ameitekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama hicho kwa asilimia 100.
Naye Mbunge Katambi,amesema yeye ni Mbunge wa Maendeleo, na dhamira yake kubwa ni kuendelea kuibadilisha shinyanga ili kuelekea kwenye hadhi ya kuwa jiji, huku akisisitiza kwamba kwenye suala la maendeleo hua hana mchezo na ataendelea kutatua kero nyingi ambazo bado ni kikwazo kwa wananchi.
Amesema katika Kata hiyo ya Ndembezi, kwamba Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alitoa fedha katika Mikoa 8 tu, ili zijengwe shule za Sekondari za Wasichana, ambapo alipambana ili kuhakikisha Shinyanga na yenyewe ina kuwemo na hatimaye akafanikiwa na kujengwa shule hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Katambi ameahidi kwamba,ataendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo wananchi wameziwasilisha kwenye mkutano wake wa hadhara, likiwamo tatizo la ufunguaji wa barabara mpya, pamoja na kuzifanyia matengenezo zile ambazo zimeharibiwa na mvua.
Katambi bado anaendelea na ziara yake ya Kata kwa Kata, huku akiwa ameambatana pia na Wataalamu wa Halmashauri pamoja na Taasisi za Serikali, ili kutoa majibu kwa wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza na wananchi wa Ndembezi kwenye mkutano wa hadhara.
Diwani wa Ndembezi Victor Mmanywa akizungumza kwenye mkutano.
Wananchi wa Ndembezi wakiwa kwenye mkutano wa Mbunge Katambi.
Mkutano wa Mbunge Katambi ukiendelea.
Post a Comment