Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media
Watu sita wote wakiwa ni wakazi wa korogwe mkoni Tanga wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shillingi milioni Moja Kwa Kila mmoja kwa kosa la kucho basi mali ya kampuni ya saibaba kinyume cha sheria
Akisoma shitaka hilo mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Francisca Maguiza, Mwanasheria wa Serikali Sarah Wangwe amesema washtakiwa hao walitenda kosa la hilo Februari 17, 2024 katika eneo la Shamba Darasa, Kijiji cha Msambiazi kata ya Mtonga wilayani Korogwe.
Waliokutwa na hatia ni Bashiru Shehoza, Bakari Anania, Bakari Mhando, Ramadhani Malaba, Benjamin Shehoza na Abdallah Koko wote wakazi wa Korogwe.
Hata hivyo, Hakimu Maguiza amesema watuhumiwa hao wana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 au kuendelea kutumikia adhabu hiyo.
Post a Comment