Na Costantine Belnardo, Misalaba Media
Afisa Programu wa Mafunzo, Uhamasishaji, na Uelimishaji Jamii kutoka Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Chanjo Lotalis Gadau amesema Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watoa Huduma za Afya juu ya uboreshaji wa Mawasiliano kati ya Mtoa huduma na Mteja "Interpersonal Communication-IPC" yatarahisisha kuongeza ufanisi katika Huduma za chanjo.
Bi. Gadau aliyamesema hayo Jana 15, Februari, 2025 Mjini Kateshi wakati wa kuhitimisha Mafunzo hayo Hamashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
“Kwanza Kabisa nitoe Shukrani kwa Ushirikiano wenu kwa kushiriki Mafunzo haya, ni matumaini yangu kuwa baada ya kupata Mafunzo haya ya siku mbili tutaongeza ufanisi Huduma za chanjo maana ukiimarisha Mawasiliano na mpokea huduma kutakuwa na matokeo chanya"amesema Gadau
Aidha kwabupande wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang
Dr.Mohammed Kodi amesema Sasa ni wakati wa kutafari kwa kila mtoa Huduma za Afya afanye mbinu zipi katika kuleta ufanisi Huduma za chanjo.
Hatahivyo ameishukuru Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo kwa kufanikisha Mafunzo hayo katika Halmashauri hiyo.
Ikumbukwe kuwa Chanjo huokoa maisha na hukinga maradhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwa ni pamoja na Surua, homa ya ini (hepatitisi B), dondakoo, Kifaduro, Nimonia, Polio, kuhara kunakosababishwa na virusi vya rota, Rubela na Pepopunda.
Post a Comment