" MAJALIWA: CCM NA SERIKALI ITAWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI NA UAMINIFU

MAJALIWA: CCM NA SERIKALI ITAWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI NA UAMINIFU

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Feb 16, 2025 amefika katika Jimbo la Maswa Mashariki, wilayani Maswa Mkoani Simiyu kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa dharura kwa ajili ya kuwalisilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Katika Hotuba yake, Majaliwa amesema Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwahudumia Wananchi kwa Weledi, Uaminifu na Uadilifu mkubwa.

Amesema serikali inagombana na Watendaji ili fedha za miradi ziweze kutumika vizuri katika kutekeleza miradi ya Maendeleo na kuhudumia wananchi ambao wanahitaji kupata huduma za kibinadamu kila siku.

"Endeleeni kumwamini Dkt. Samia ambaye anaendelea kuwaletea fedha za miradi ya Maendeleo, CCM imedhamiria kuwatumikia Watanzania wote kila eneo amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amewataka viongozi wa CCM, wilaya ya Maswa kuhakikisha wanapita vijijini kwa ajili ya kunadi miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwaaminisha wananchi kuwa CCM na sera zake itaendelea kuleta maendeleo kwa Uaminifu.

Pamoja ma mambo mengine, Majaliwa amesema Mkoa wa Simiyu unaongoza kwa uzalishaji wa Pamba na kwamba serikali imejiimarisha kuzalisha kwa tija na uwepo wa viwanda vingi vya Pamba Mkoani humo utaongeza tija na thamani ya Pamba.




 




Post a Comment

Previous Post Next Post